VETERINARY PROFESSIONAL

  • Home
  • Download App
  • Surgery
  • Medicine
  • Pharmacology
  • Parasitology
Home » NEWS » Sekta ya mifugo mkoa wa Dar es Salaam

Saturday, March 22, 2014

Sekta ya mifugo mkoa wa Dar es Salaam

Utangulizi
 
Katika Mkoa wa Dar es Salaam upo ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali kwa wanyama wakubwa na wadogo, kwa ajili ya chakula , biashara, wanyamakazi na wanyama rafiki (pets). Shughuli za ufugaji zinafanyika kwa idadi maalum kutegemeana na aina ya mifugo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Aidha ufugaji huu unasaidia kwa kiwango kizuri kutoa ajira kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ufugaji huu unatakiwa uwe endelevu na wenye kuzingatia kanuni za ufugaji bora.
 
 
 
Huduma za ugani:
 
Huduma za ugani hutolewa na wataalam wa mifugo wa Serikali wa Halmashauri za Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na sekta binafsi katika klinik na vituo vya mifugo.
 
 
Indigenous cattle keeping are not prominent in the region. These supply the draught animals and others are reared for slaughtering and milk. In some periods few cattle are brought in from other regions for fattening and then slaughtered or exported to Arabian countries and Comoro. The region slaughters an average of 800-1000 cattle daily 
 
 
Huduma zinazotolewa na Wataalamu wa Mifugo wa Serikali:-
  1. Kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo
  2. Kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji kuhusu kanuni za ufugaji bora
  3. Uhamilishaji (A.I.) na kupima mimba
  4. Ukaguzi wa nyama na ngozi
  5. Kutoa vibali vya kusafirisha mifugo
  6. kutoa vibali kwa watu walioumwa na mbwa/wanyama kuweza kupata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kichaa cha mbwa katika hospitali za binadamu.
 
Huduma zinazotolewa na wataalam wa sekta binafsi:
 
1.  Kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo
2.  Kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji kuhusu kanuni za ufugaji bora
3. Uhamilishaji (A.I.) na kupima mimba 


Uuzaji wa mifugo katika mnada wa Pugu
 
Mnada wa upili wa mifugo (secondary market) wa Pugu, unapokea wastani wa ng'ombe 451 , mbuzi na kondoo kwa pamoja 130 hadi 400 kwa siku
 
 
Viwanda vya kusindika maziwa na bidhaa zake:
 
 
1.Royal Dairies
2. Azam Dairies
3.Tomy Dairies
4.Tan Dairies

 
Viwanda hivi vinasindika maziwa na kutoa mazao mbalimbali kama vile siagi, jibini, mtindi, na maziwa freshi. Maziwa yanayosindikwa hupatikana toka kwa wafugaji walioko mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Mazao ya mifugo

Mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka huzalisha wastani wa vipande vya ngozi za ng'ombe 194,489 , mbuzi 72,788 na kondoo 18,948 . Yapo makampuni 4 yanayojishughulisha na ununuzi wa ngozi moja kwa moja au kupitia kwa wafanyabiashara wa ngozi kutoka machinjio za mkoa wa Dar es Salaam, kati yao kampuni 1 inajishughulisha pia na usindikaji wa ngozi. Makampuni hayo ni:-
  1. East Africa Leather Company
  2. Afro Leather Company inajihusisha na ununuzi pamoja na usindikaji wa ngozi.
  3. SAK International
  4. Lake Traders Company
Mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka huzalisha wastani wa tani za maziwa 17,739 na mayai trei 1,440,000 .Uzalishaji wa nyama kwa mwaka ni wastani wa kilo 32,118,844 kwa aina mbalimbali za wanyama kama inavyooneshwa katika jedwali:-
Na. Aina ya mifugo Kiasi cha nyama (Kg)
1 Ng'ombe
28,246,500
2 Mbuzi
1,136,496
3 Kondoo
178,644
4 Nguruwe
736,500
5 Kuku
1,820,704
  Jumla
32,118,844

Bonyeza hapa kujua takwimu mbalimbali za Mifungo na mazao yake katika Mkoa wa Dar es Salaam.
f
Share
t
Tweet
g+
Share
?
Unknown
11:02:00 AM
Newer Post Older Post Home
Find Us :

Translate Here

Popular posts

  • Vector & Vector-Borne Diseases Research Institute (VVBDI)
    INTRODUCTION The Vector and Vector-Borne Diseases Research Institute (VVBDI) which was previously known as Tsetse and Trypanosomiasis R...
  • LIVESTOCK EXTENSION GUIDELINE
    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA MINISTRY OF LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT LIVESTOCK EXTENSION SERVICES IMPLEMENTATION GUIDELINES...
  • PROLAPSE IN CATTLE
    A prolapse can be basically defined as an abnormal repositioning of a body part from its normal anatomical position. Two distinct types of...
Powered by Blogger.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Followers

AD (728x90)

Call

Skype Me™!

Featured Posts

Copyright 2013 VETERINARY PROFESSIONAL - All Rights Reserved
Design by Mas Sugeng - Published by Evo Templates