VETERINARY PROFESSIONAL

  • Home
  • Download App
  • Surgery
  • Medicine
  • Pharmacology
  • Parasitology
Home » NEWS » VETERINARY NEWS » Mtanzania agundua chanjo ya ndui ya kuku

Wednesday, June 25, 2014

Mtanzania agundua chanjo ya ndui ya kuku

Dar es Salaam.  Tanzania imeingia katika vitabu vya kihistoria ya tiba baada ya Profesa Philemon Wambura kugundua chanjo ya ugonjwa wa ndui kwa kuku ambayo imetambuliwa kimataifa.
Chanjo hiyo iitwayo ‘Fowl Pox TPV-1 strain,’ iliyofanyiwa utafiti kwa miaka 10 na ya kwanza kugunduliwa duniani, itaanza kutumika Afrika na dunia nzima hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano na kampuni ya kimataifa  inayotengeneza dawa na chanjo mbalimbali za mifugo, MCI Sante Animale ya Morocco, Profesa Wambura alisema chanjo hiyo ni ya kwanza kukubalika kutumika kuzuia ugonjwa wa ndui ya kuku na ni rahisi kutumia ukilinganisha na chanjo nyingine zilizowahi kufanyiwa majaribio.
“Ni fahari kwa Tanzania kuwa mgunduzi wa kwanza wa chanjo hii duniani, ni chanjo yenye ubora wa hali ya juu  na matumizi yake yataongeza uzalishaji wa kuku na kuongeza kipato,” alisema Profesa Wambura ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Tiba ya Wanyama wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA).
Profesa Wambura alisema tofauti na chanjo nyingine, hiyo inaweza ikawekwa kwenye chakula au maji ya kunywa bila kupata usumbufu wa kuwakamata mmoja mmoja na kuweka dawa machoni kama ilivyozoeleka.
Alisema chanjo hiyo ina sifa kubwa ya kuvumilia joto, jambo linaloifanya kuwa ni rafiki wa mazingira ya vijijini ambako hakuna umeme na ina uwezo wa kutambua iwapo kuku ana virusi vya ugonjwa wa ndui kwa kutumia damu ya kuku mwenyewe.
“Madhumuni yetu ni kuhakikisha chanjo hii inapatikana kwa bei nafuu ili hata wananchi wa kawaida wanufaike. Ndiyo maana itazalishwa kwa wingi ili iuzwe kwa bei nafuu,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk Hassan Mshinda alisema ni fahari kubwa kuwa kazi ya mtafiti wa Kitanzania imeonekana na mataifa ya nje, jambo ambalo linatoa ari kwa watafiti wengine kufanya kazi zaidi.
Alisema mradi  huo wa chanjo ya ndui ya kuku uliogharimu Sh205 milioni ni wa kimataifa na chanjo hiyo itasambazwa duniani kote kwa ushirikiano wa Costech na Kampuni ya MCI.
“Ni vizuri sasa tafiti za Kitanzania zinatumika badala ya kuhifadhiwa kwenye makabrasha bila faida yoyote. Ni kazi ya kujivunia hasa,” alisema
Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji wa Biashara wa MCI, Dk Baptiste Dungu alisema kampuni yake imefanya kazi na Profesa Wambura na kugundua kuwa utafiti wa chanjo yake una manufaa makubwa kwa sababu ni wa kwanza duniani.
SOURCE MWANANCHI
f
Share
t
Tweet
g+
Share
?
Unknown
6:50:00 AM
Newer Post Older Post Home
Find Us :

Translate Here

Popular posts

  • GET TO KNOW THE HIGH AND LOW MAINTENANCE PETS
    GET TO KNOW THE HIGH AND LOW MAINTENANCE PETS 1.) High-maintenance pets (not ranked in any particular order) Dogs Dogs can require more or ...
  • Treatment of complete vaginal prolapse
    Treatment of a mild early prolapse may require only simple cleaning of exposed tissues, application of ointment eg Hibitane cream or petro...
  • PROLAPSE IN CATTLE
    A prolapse can be basically defined as an abnormal repositioning of a body part from its normal anatomical position. Two distinct types of...
Powered by Blogger.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Followers

AD (728x90)

Call

Skype Me™!

Featured Posts

Copyright 2013 VETERINARY PROFESSIONAL - All Rights Reserved
Design by Mas Sugeng - Published by Evo Templates